Serikali Yatoa Mwongozo Mpya Kupambana Na Corona
Serikali kupitia Wizara ya Afya imewataka wananchi kuendelea kujikinga na Corona kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ikiwemo kuvaa barakoa kwenye ofisi zote za serikali, shule na taasisi mbalimbali ikiwemo hospitali.
Muongozo huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo leo Julai 4, 2021, jijini Dodoma ambapo amesisitiza kuwa mamlaka zihakikishe kuna miundombinu ya maji tiririka, sabuni au vitakasa mikono ili wananchi, wanafunzi, wagonjwa waweze kuvitumia.
Aidha Prof. Makubi ameongeza kuwa mwongozo huo unatakiwa kufuatwa shuleni, vyuoni na kwenye taasisi mbalimbali za elimu na hospitali ikiwemo kuweka miundombinu inayowezesha kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kuvaa barakoa muda wote.
No comments