Header Ads

Header ADS

Polisi Mtoro Kenya Aliyekuwa Akisakwa kwa Mauaji Apatikana Amekufa




Afisa mmoja wa polisi ambaye amekuwa mafichoni baada ya kuwaua watu wawili amepatikana ameaga dunia.

Mwili wa polisi huyo ambaye amekuwa akisakwa baada ya kuwaua watu wawili,umepatikana nyumbani kwa wazazi wake kaunti ya Elgeyo Marakwet eneo la Rift Valley.

Kulingana na polisi afisa huyo alimpiga risasi mwenzake John Ogweno Jumatatu tarehe 5 Julai na kisha kutorokea eneo la Juja viungani mwa mji wa Nairobi alipomuua mwanamme mwingine aliyetambuliwa kama Peter Ndwiga kwa kumpiga risasi katika chumba cha malazi hotelini.


No comments

Powered by Blogger.