Header Ads

Header ADS

Mafia Hushpuppi Kwenda Jela Miaka 20





Mwamba anayetajwa kuwa ni Mafia namba moja nchini Nigeria kwa kuiba pesa mitandaoni, Ramon Abbas almaarufu Ray Hushpuppi amekiri kuwa ana kosa katika makosa ya kutakatisha pesa na utapeli wa mitandaoni.

 

Hushpuppi; mkali wa udukuzi alikuwa tishio mitandaoni kwa kula bata na kuvaa nguo za ghali kiasi cha kubatizwa jina la Gucci Master, lakini sasa huwenda akatumikia kifungo cha miaka 20 jela.



Kwa mujibu wa mwandishi maarufu nchini Marekani, Evan Ratliff wa Shirika la Habari la Bloomberg, Hushpuppi amekiri kuwa na hatia mahakamani kwa kuhusika katika utakatishaji wa pesa kutoka kwenye utapeli wa kutumia e-mail na wizi mwingine wa mitandaoni.

 

Jamaa huyo amekiri kutakatisha pesa katika benki mbalimbali duniani ikiwemo nchini Malta. Pia anadaiwa kutaka kutapeli moja ya timu za Ligi Kuu Uingereza kwa njia ya e-mail pamoja na kutaka kutapeli kampuni ya wanasheria ya Marekani.



No comments

Powered by Blogger.