Kajala Atema Nyongo Kwa Wanaomsema Mitandaoni!
SUPASTAA mwenye mvuto kunako Bongo Movies, Kajala Masanja au Mama Paula ametema nyongo laivu.
Kajala amesema kuwa, baadhi ya watu wanapoamua kumsema kila kukicha kwenye mitandao yeye na mtoto wake, Paula Kajala, basi wajue wanazidi kumuongezea siku za kuishi hapa duniani.
Anasema kuwa, hii ni kwa sababu wanaofanya hivyo hawahangaiki na vitu vyao vinavyowahusu, badala yake wako bize na mambo yake na mwanawe.
Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Kajala anasema kuwa, anawashangaa watu wengi wameacha kazi zao zinazowahusu za kila siku badala yake wako kwenye mitandano kumtukana yeye na mtoto wake, jambo ambalo linamshangaza, lakini analifurahia kwa sababu wanamuongezea siku za kuishi.
“Unaju mtu akiwa anasemwa kila siku bila sababu za msingi; yaani ukiamka mtu ni kushika simu na kwenda kwenye mitandao kunitukana mimi na mtoto wangu, Mungu anawashangaa sana na ananipa zawadi ya kuniongezea siku za kuishi na mtoto wangu, maana ameshaona watu hawawezi maisha yao mengine bila mimi na mtoto wangu,” anasema Kajala.
Kajala amekuwa akiandamwa juu ya malezi ya mwanawe, Paula wakimtuhumu kumuingiza kwenye mambo ya kikubwa angali bado na umri mdogo wa miaka 19, tayari yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny.
No comments