Corona yaitikisa Manchester United
MANCHESTER United imelazimika kusogeza mbele mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Preston North End uliotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi kutokana na kutikishwa na janga la Corona.
Inaelezwa kuwa kuna wachezaji tisa wa Manchester United ambao wamepata Virusi vya Corona jambo ambalo limezua hofu na kuamua kuchukua tahadhari.
Vipimo vilivyochukuliwa kufuatia mechi ya kirafiki ya juzi Jumatano dhidi ya Brenford ambayo ilichezwa mbele ya mashabiki 30,000, vilionyesha idadi hiyo ya waathirika katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkjaer.
Mechi hiyo ya Jumatano iliisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2. Pia mechi ya Bretford dhidi ya West Ham inaweza isichezwe kwa kuwa Brendford nao wanafanya vipimo kutokana na kuhusika na mchezo dhidi ya United.
Taarifa kutoka United jana ilieleza kuwa kuendeleza usalama dhidi ya Corona ndiyo kipaumbele chao jambo ambalo limefanya waliopata Corona wajitenge na wengine.
"Kufuatia vipimo vya wachezaji wa kikosi cha kwanza tumepata idadi ndogo ya waathirika hiyo imefanya wengine kujitenga wakisubiri vipimo zaidi,".
No comments