Header Ads

Header ADS

Wema Sepetu Amuonea WIVU Jack Wolper Kupata Mtoto


Baada ya kusambaa kwa habari kuwa wolper anatarajia kupata mtoto, pongezi na hongera zilikuwa nyingi sana kwake baada ya kuthibitishwa kwa taarifa hiyo kwenye ukurasa wa mpenzi wake @richmitindo

Ikumbukwe Kulikuwa na habari nyingi sana na maneno mengi juu ya ishu nzima ya Mrembo Wolper kutokuwa na ujauzito, suala ambalo kila mtu amekuwa akiliongelea kwa stahili yake huku wengine

wakifikia hatua ya kumkejeli

Leo kupitia ukurasa wa instagram wa staa wa film nchini @wemasepetu amelitolea uvivu swala hilo kwa kuandika ujumbe ulioashiria kuwa amepatwa na wivu baada ya mrembo huyo kushika ujauzito na kumuacha peke yake katika kundi la Warembo ambao bado hawajabarikiwa kupata Ujauzito

"Nilivyosikia kwa mara ya kwanza nikawa kama siamini amini... Kwakua ni mengi huwa tunaongeaga na hatufichani basi katika maongezi yetu ya hapa na pale nikaamua kukuuliza kama swali la kizushi & nakumbuka ulinikatalia... Basi karoho kangu kakatulia na kupoa... Maana nikaona , "Hee, Mzee mwenzangu tena mambo gani haya anataka kuniacha peke yangu kwenye hili kundi tena jamani..." 🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️😂😂🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️

Sasa ilipofikia point maneno yakawa mengi kuhusu tumbo... Nikarudi tena kwa mara ya pili sasa nikiwa sina uhakika saana na majibu yako maana kwanza ulipotea, ukawa hata kwenye shughuli sikuoni so kama mtu mzima nikaunganisha Dots na pia nilikuelewa saana dhumuni la kufanya siri... Wivu ulikuwepo kwa saana ila pia niliamini kuwa Mungu kweli anakupa kwa wakati na nikawa sooo happy & excited for you...

Baada ya kusikia umejifungua na nilivyokupa hongera na ukasema Asante kamoyo kalichoma kama pasi nikijua sasa ni kweli nimeachwa mwenyewe ila ukanipigia mstari ile kauli ya "Wakati wa Mungu" na kwa namna moja au nyingine nikapata Faraja kidogo kutokana na maneno mengi mazuri ulioniambia...Leo hii unaitwa Mama my Love... Umepata furaha yako ya Ukweli... Naomba Mungu akakukuuzie kipenzi cha roho yako vyema na afya thabiti... I cannot wait to see his cute little self.... Mashallah... Hongera nyingi sana zije kwenu Mommy P & Daddy P.... Allah Barik...

Iam Extremely Happy for you two... Tumachozi sasa.... Natufuta kwa mbali... 🥺🥺🥺" ✍️......@wemasepetu



No comments

Powered by Blogger.