Ukweli Unauma: Wanawake Wanavyopambana Kujikwamua Kiuchumi Ndoa Nyingi Zinazidi Kuingia Matatizo
Kadiri wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndivyo ndoa nyingi zinazidi kuingia matatizoni. Tatizo sio wao kupambana bali tatizo liko hapa:
Wanapambana kwa madhumuni gani? Wanawake wengi hawapambani kwa maana ya kuwasaidia waume zao [kama Mungu anavyotaka] bali kwa maana ya kutoka kivyao; ndio maana utawasikia wanaongea kauli zao za kiuanaharakati, "Usimtegemee mume", "wanaume hawaaminiki", "bora mwanamke niwe na uchumi wangu n.k".
Hivi mnajua kuwa...
Kama mume ni kichwa maana yake mke ni kiwiliwili; bahati mbaya ni kwamba macho na ubongo viko kwenye kichwa na sio kiwiliwili. Kiwiliwili kisipokiamini kichwa "automatic" kitaielekeza miguu kokote na kwa kuwa hakuna macho kuna mawili; mwili(ndoa) kuumia kutokana na kujikwaa ama kufa kabisa kwa kutumbukia shimoni.
Ngoja niwambie; ndoa yeyote ambayo mwanamke amekaa kiuanaharakati uwe na uhakika ilishajifia siku nyingi ama iko njiani kufa na ukiona wanandoa wanaendelea kuishi pamoja basi ujue ni kwa "kujilazimisha". Sijakutana na mwanamume yeyote duniani ambae anaweza kuishi kwa furaha nyumba moja na mwanamke anaeleta tabia za uanaharakati ndani ya ndoa.
Nataka ufahamu...
Ukiruhusu mwanamke ndani ya ndoa ajione anaweza kusimama bila wewe (mumewe) basi, ujue unacheka na nyani na muda wowote tutakuja tukusanye mabua tukalishie ng'ombe wetu. Kuishi na mke hakuhitaji DEMOKRASIA, kunahitaji AKILI, ujinga unaofanywa na wanaume wengi siku hizi ni kuruhusu DEMOKRASIA kutawala ndoa badala ya AKILI. Wewe kama unadhani demokrasia ndio uzungu na mapenzi kwa mkeo, shauri yako; hao wazungu unaowaigilizia ndoa zishawakimbiza siku nyingi.
Msifanye mchezo wandugu...
Ninawaonya mapema ili nisije kusikia eti mtu ananiambia mke aliemtafuta na kumuoa mwenyewe, amemshinda! Khaa! Yaani hapo itabidi utandikwe viboko vya mgongo; maana unakuwa umemdhalisha Mungu na umeudhalilisha uanaume pia. Uanaume tafsiri yake ni "Kuishi na mwanamke kwa akili kiasi kwamba abaki akikuheshimu na kukunyenyekea kwa furaha". Ukiona mwanamke anakudharau na hakusikilizi basi ujue umeshapoteza uanaume wako.
Andika hii pointi mahali...
Elewa kwamba uanaume haukai kwenye suruali bali uanaume unakaa kwenye akili.
By Bujibuji

No comments