Shaffih Dauda "Mtazamo WANGU Tukio la Jana Mechi ya Simba na Yanga Kuhairishwa"
Awali niwape pole Mashabiki, wadau, timu zote mbili na Wanafamilia wote wa mpira wa miguu nchini Tanzania, niwape pole kwa Wafanyabishara, Watu wa Media na makampuni yote yanayowekeza pesa kwenye mpira huu
Niwape pole wale wote wanaofanya jitihada za makusudi kuhakikisha mpira wetu wa miguu unasonga mbele, ijapo bado kuna mkwamo mkubwa kwenye harakati hizi ila nawaomba tutumie jana kama funzo la kusonga mbele
Binafsi nimeitazama vyema barua ya Shirikisho kwenda kwa Klabu na taarifa kwa umma, kama nimeielewa vyema ile taarifa haikutoa sababu halisi ya mchezo kusogezwa mbele, hilo ni kosa la kwanza, sababu ni muhimu kwakuwa mpira ni biashara pia
Lakini baada ya TFF na Bodi kupokea taarifa kutoka kwa Wizara, kuna shida ya ufikishaji wa ile taarifa, Wizara ya Michezo haiwezi kusogeza mchezo wa mpira mbele, bali kutoa ushauri na kusikilizana pande zote husika
Mwisho barua inasema taarifa ilifikishwa kwa klabu, huenda ni kweli ila walitoa nafasi ya kujadiliana? Serikali ni Mdau, TFF ni Mama, Simba na Yanga ni wadau hizo ndio pande zilizopaswa kukaa mezani kujadiliana na sio kufikisha tu taarifa
Liverpool na Manchester United kabla taarifa kutolewa kwa umma, waliitwa wote wawili, iliitwa Bodi ya Ligi na Chama pamoja na Mamlaka zote kujadiliana, Yanga kasimamia kanuni huenda TFF hawakutoa nafasi ya majadiliano, shida inaanzia hapo
Sheria na Kanuni imesimamiwa ila hii hii kanuni inaweza kupindishwa kama mtajadiliana (Collaborative decision), tafsiri siku zote ya sheria haijawahi kutaka haki bali sheria inataka Mshindi tu, Yanga katafsiri kanuni na sheria, thats all
Wizara ina mamlaka kwenye nchi, TFF ni Mama ila klabu zinamiliki Mashabiki, ile picha ya Yanga kuondoka na Mashabiki wao ni tafsiri halisi ya FOOTBALL IS FOR THE FANS, kwenye maamuzi yoyote makubwa ni lazma TFF wapime na kujadiliana
Mwisho, Mashabiki wameonewa kwenye hili, kwanza pesa zao achana tiketi vipi nauli, malazi na makazi? Nani atawalipa? Heshma yetu ya mpira itarudi vipi kimataifa? Kwenye hili suala busara inahitajika sana ili huu mpira uwe na nguvu tena
Even the Gods, find it difficult to love and to be wise
No comments