Roketi la China latarajiwa kuingia anga ya dunia leo
Sehemu kubwa ya roketi ya China inatarajiwa kuingia tena katika anga ya dunia mapema hii leo, wakati China ikiondoa wasiwasi juu ya madhara yake.
Wataalamu wanasema ni vigumu kutabiri aina hiyo ya roketi Long March -5B itaingia eneo jipi na muda gani katika anga ya dunia.
Mamlaka za China, zilisema kwa kiasi kikubwa roketi hiyo itaharibika itakapokuwa ikianguka. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin aliwaeleza waandishi wa habari siku ya Ijumaa kwamba uwezekano wa roketi hiyo kusababisha madhara ardhini ni mdogo sana.
Ingawa kumekuwa na uvumi juu ya mahali ambapo roketi hiyo au vipande vyake vinaweza kuanguka, lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya vipande ambavyo havitaharibika basi vinaweza kuanguka baharini.
No comments