Ninja: Nipo Tayari, Mleteni Yeyote
BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema kuelekea mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Simba yupo tayari kukabiliana na mshambuliaji yeyote wa Simba.
Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 61 walizopata kupitia michezo 57 wakati Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 57 kwenye mechi 27, timu hizi leo zitakutana kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara na mechi yao ya mwisho iliisha kwa sare ya bao 1-1.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ninja ambaye ana nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza leo alisema kuwa: “Tumejiandaa vizuri kama timu nzima, maana uwanjani sijajua nitakabana na nani na uwanjani kuna mambo mengi tumejipanga timu nzima kukabiliana nao.
“Tunacheza na timu kubwa na yenye wachezaji wazoefu ila kwa uwezo wa Mungu na kwa kufuata maelezo ya mwalimu tutafanya vizuri.”
STORI: CAREEN OSCAR ,Dar es Salaam
No comments