Ndugai: Mnaogopa Nini Kuleta Viambatanishi Ili Tuwavue Ubunge?
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameendelea kutoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa kuwavua ubunge wabunge 19 wa viti maalumu wa CHADEMA, Mh Spika ameendelea kusisitiza kuwa anaongoza Bunge kwa Katiba, Sharia, Kanuni, Hekima na Utamaduni ili kutenda haki.
Mh Spika amevitaka vyama vya siasa pale wanapotaka kuwavua uanachama wabunge yawapasa kuambatanisha Katiba ya chama chao pamoja na Muhtasari wa Kamati Tendaji ya chama iliyofanya maamuzi ya kuwavua uanachama wabunge wanaopaswa kuwafukuza ili naye apate kujilidhisha kama utaratibu ulifuatwa na atende haki pasi kumuonea mtu yeyote.
Mh Spika ameongeza kuwa kwa mujibu uo atafanyakazi pia na msajiri wa vyama vya siasa maana yeye ndo ana Katiba za chama na kila wanapofanya mabadiliko ya Katiba kwenye vyama ua anapelekewa nakara za katiba ambazo ni latest. Mh Spika amemalizia kwa kuhoji kwanini Chadema hawapeleki hizo nakala? Wanaogopa nini?
No comments