Melinda Gates Atajwa na FORBES kuwa BILIONEA mpya Baada ya Kuingiziwa Kiasi Cha Trilioni 4.1 na Bill Gates
Siku tatu baada ya kuachana na mumewe Bill Gates, Jarida la Forbes limemtangaza Mwanamama Melinda Gates kuwa BILIONEA mpya, hii ni mara baada ya kuhamishiwa kiasi cha ($1.8 BILLION) takribani TZS. Trilioni 4.1 toka kwenye kampuni ya Bill Gates kama mnufaika wa hisa za uwekezaji.
Kampuni ya bilionea Bill Gates (Cascade Investment) imeripotiwa kuhamisha kiasi hicho cha fedha Jumatatu (Mei 3) siku ambayo wawili hao walitangaza kutalikiana. Utajiri wa Bill Gates umeshuka toka ($130.4 B) hadi ($128.6 B) baada ya kuhamishwa kwa fedha hizo, lakini bado inamuweka Bill nafasi ya 4 kwenye orodha ya matajiri wa dunia.
Melinda sasa ni mnufaika wa mamilioni ya hisa ikiwemo 14.1 million za Kampuni ya Taifa ya Reli nchini Canada, hisa ambazo zina thamani ya ($1.5 Billion) pia amenufaika na hisa za kampuni ya AutoNation ambao wao wamehamisha kiasi cha ($309 million) kwenye hisa za Melinda zilizofika 2.94 million. Kwa pamoja ndio unapata kiasi cha ($1.8 Billion)
No comments