Mchezaji EDEN Hazard Aomba Radhi
Mshambuliaji wa Real Madrid, Eden Hazard ameomba radhi kwa kitendo cha kucheka na wachezaji wa Chelsea baada ya timu yake kutolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya.
"Huwezi kuona mchezaji kama Ronaldo akifanya hivi baada ya kutolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya" Moja ya ujumbe ulioandikwa na shabiki wa Real Madrid kuhusu Hazard.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa maika 30, alionekana akifanya mzaha na kucheka na wachezaji wenzake wa zamani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya ligi ya nabingwa barani ulaya.
Hazard aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba haikua nia yake wala hakufanya vile ili kuwakera mashabiki wa Real Madrid.
Hazard alifanyiwa mabadiliko kwenye mchezo huo kabla ya mchezo kumalizika ambao miamba hiyo ya Uhispania ilipoteza kwa kufugwa magoli 2- 0 na Chelsea kufuzu hatua ya fainali.
Hazard ambaye aliondoka Stamford Bridge mwaka 2019, amepata lawama nyingi kutoka kwa mashabiki wa Real Madrid na vyombo vya habari vya Uhispania, wengine wakitaka aondolewe klabuni hapo.
No comments