Header Ads

Header ADS

Kumekucha.. Zari Aipasua Familia Ya Mondi





UNAIKUMBUKA ile vita ya Team Zari na Team Wema? Timu hizi zilikuwa zikiwapigania mastaa hao; kila moja ilimuona mtu wake ndiye mwenye haki ya kuwa mpenzi wa mkali wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, lakini sasa mambo yamebadilika, IJUMAA limedokezwa.Kwa sasa mtiti umehamia kwa wazazi wenza wa Diamond au Mondi, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady ’ na Tanasha Donna ambao wanatajwa kuipasua vipandevipande familia ya staa huyo wa Wimbo wa Waah.

 

MOYO WA MONDI KWA ZARI

Wakati Mondi akidaiwa kuwa moyo wake upo kwa Zari ambaye amezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan, upande mwingine wa familia upo kwa Tanasha.Mara tu baada ya Mondi kutinga nchini Afrika Kusini (Sauzi) hivi karibuni, stori kubwa ni juu ya kurudiana na Zari kufuatia kutinga nyumbani kwake na kuonekana akivinjari na watoto wake hao.



Mbali na kujiachia nyumbani kwa mwanamama huyo, kubwa kuliko ni kusambaa kwa picha zake na Zari wakiwa kimahaba, kiasi cha baadhi ya watu; hasa Team Zari kupiga kelele tatu wakiamini wamerudiana.

 

Hata hivyo, bado wenyewe hawajajitokeza hadharani kuthibitisha kama wamerudiana, lakini mamilioni ya wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii waliotamani siku moja wawaone pamoja, roho zao zipo kwatu.

 

Mondi yupo Sauzi akiandaa albam yake mpya ya muziki itakayoingia sokoni baadaye mwaka huu.Vyanzo vya ndani ya familia ya Mondi vinathibitisha kwamba, kwa takriban miaka mitatu tangu jamaa huyo alipotengana na Zari siku ile ya Wapendanao ya Februari 14, 2018, amekuwa akikiri waziwazi kwamba, hajawahi kupata mwanamke aliyekamilika na mwenye vigezo vya kutosha vya kuwa mke kama Zari.

 

Ikumbukwe kwamba, Mondi amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake kadhaa maarufu, lakini Zari amehusishwa naye siku zote na yeye mwenyewe Mondi hajawahi kukaa kimya kwa kila alipotakiwa kumzungumzia mama huyo wa watoto watano alisema; “Hatujarudiana, lakini mbali na kuwa mzazi mwenzangu, niseme wazi kwamba ni mwanamke mwenye vigezo vyote na aliyekamilika kila idara.



”MAMA DANGOTE ANAMTAKA TANASHA

Katika kuthibisha kwamba kuna mpasuko kwenye familia ya Mondi, mama mzazi wa staa huyo, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ amekuwa akionesha ishara zote za kumtaka Tanasha ndiye awe mkwe wake.Vyanzo vya ndani ya familia vinathibitisha pasi na shaka kwamba, Mama Dangote anampenda zaidi Tanasha ukilinganisha wanawake wengine wawili waliozaa na Mondi; Zari na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

 

Gazeti la IJUMAA lina data za ndani zinazoonesha kwamba, Mama Dangote anamkubali na kumpenda Tanasha.Inadaiwa kwamba, Mama Dangote amekuwa akitumia nguvu nyingi mno katika kumsihi Mondi arejee kwa Tanasha.Miezi kadhaa iliyopita, Gazeti la IJUMAA lilinasa habari za ndani za Mama Dangote kufanya mawasiliano na Tanasha akimtaka kurejea Bongo yeye na mwanawe aliyezaa na Mondi, Naseeb Junior.

 

Habari hizo zilivuja baada ya Mama Dangote kuvujisha video ya Mondi akizungumza Naseeb Junior.Pia Mama Dangote alivujisha video nyingine ambayo Mondi alikuwa akimuimbia Tanasha enzi za penzi lao motomoto mara tu baada ya kujaaliwa kumpata mtoto huyo.

 

Matendo hayo ya Mama Dangote ndiyo yaliyoanza kutengeneza picha kwamba huwenda anatamani Tanasha angerejea kwenye himaya ya mwanawe huyo kwani hata kuachana kwao hakukuwa na sababu kubwa kihivyo.Katika kuthibitisha kwamba, hisia hizo za baadhi ya watu zilikuwa za kweli, mwezi mmoja mara tu baada ya Zari kutinga Bongo kuwaleta Tiffah na Nillan, Mama Dangote alidaiwa kumuita Tanasha ambaye naye alitua Bongo.

 

Mwezi mmoja baadaye, Tanasha alikuja Bongo kwa madai kama ya Zari (kumleta mtoto), lakini ishu ilikuwa ni namna alivyopokelewa na watu wengine, tofauti na Zari ambaye alipokelewa na Mondi mwenyewe.Kama kweli Mama Dangote anataka Tanasha arejee kwa Mondi, inaonesha ni kwa jinsi gani moyo wake upo kwake.Imeelezwa kwamba, Mama Dangote amekuwa akimtumia mtoto wa Tanasha kuonesha namna anavyomkubali Tanasha.

 

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA unathibitisha kwamba, siyo siri, Mama Dangote amekuwa akimposti mno mtoto wa Tanasha kwenye mitandao ya kijamii ukilinganisha na wajukuu wake wengine kutoka kwa Zari na Mobeto.

 

NDUGU WENGINE WAGAWANYIKA

Kwa upande wa ndugu wengine wa Mondi kama Esma Platnumz na Rommy Jones, wanaonesha kugawanyika kwenye ni nani sahihi kwa jamaa yao huyo.

 

Rommy Jones amekuwa akionesha waziwazi kuwa yupo upande wa Zari kutokana na namna wanavyoungana mkono kwenye mitandao ya kijamii.Esma yeye anasema yupo tayari kumkubali yeyote atakayeletewa na kaka yake huyo bila kubagua.“Mimi siwezi kumpangia, ila yeyote atakayempenda na kumkubali yeye, mimi nitamuunga mkono,” anasema Esma ambaye amepewa jina la Yuda kutokana na tabia yake ya kuwageuka wanawake wa kaka yake huyo mara tu anapoachana nao.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar



No comments

Powered by Blogger.