Header Ads

Header ADS

Kajala, Paula Waula Baada Ya Skendo Ya Harmo



WAKATI mwingine kuna changamoto ambazo unaweza kuzipitia, halafu zikawa ni ngazi ya kupandia kufikia mafanikio f’lani.

Hicho ndicho kimetokea kwa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja na mwanawe, Paula Paul ‘Paula Kajala’ ambao baada ya kukumbana na kashkashi kwenye ile skendo yao na staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, sasa wameula

Hivi karibuni, Kajala na Paula waliingia kwenye msukosuko ambao bado upo kwenye ngazi ya uchunguzi wa kipolisi wakidaiwa kusambaza video chafu iliyosemekana ni ya Harmonize au Harmo.

Kajala amelithibitishia Gazeti la IJUMAA kwamba, yeye na Paula wamelamba dili nono la kutangaza nguo kutoka Kampuni ya GSM.

“Yote ni mipango ya Mungu na ndiye mtoaji wa riziki hivyo tunamshukuru yeye,” anasema Kajala.Kufuatia ishu hiyo, baadhi ya watu wameibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, wakisema kwamba, kumbe inawezekana mtu kupitia kwenye changamoto kama ilivyokuwa kwa Kajala na Paula, halafu ikawa ni kama kumpiga chura teke na kumuongezea mwendo ambapo atajikuta amekwenda mbali zaidi.

Stori: Imelda Mtema, Dar



No comments

Powered by Blogger.