Header Ads

Header ADS

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Simba vs Kaizer Chiefs"


Mambo 10 nilioyaona Simba vs Kaizer Chiefs

1: Simba OUT.. Jasho Limevuja, Damu imemwagika. Kutoka Robo Fainali ya 2018/19 hadi 2020/21 kila shabiki wa Simba atakuwa anaondoka Kwa Mkapa, akijipa kifuani mwake. Kuna HATUA KUBWA SANA Simba imepiga.

2: Well Done kwa wachezaji wa Simba 👏 Wamepambana sana. Walionyesha Thamani ya Logo ya Simba kwenye jezi walizovaa. Kwa presha ya mechi ilivyokuwa, Ukubwa wa Kaizer, kama unapenda mpira, una kila sababu ya kuheshimu MABAO MATATU, SIMBA aliyoyafunga kwa Mkapa

3: Well done Gomes👏 Tactically, 'game plan' ilikuwa superb sana. Niliipenda sana Sub ya Muzamir kwa Morisson. Kama kuna mahala mpango wake ulikwama basi ni kwenye majukumu ya Kapombe. Kivipi?

4: Didier alitaka viungo wautembeze mpira na sio kutembea na mpira. Miquissone na Chama wakawekwa kwenye 'half Spaces' ili kutengeneza 'gape' kwa mabeki wa pembeni kupita na kushambulia. Sielewi kwanini Kapombe alichagua zaidi kupiga krosi nyingi za juu. Low Crosses zingeweza kuwa na manufaa zaidi

5: Simba wamepiga mashuti 32.. ON TARGET 10🙌 Hapa unaanza kuisifia mikono ya kipa wa Kaizer, BVUMA kisha unaelewa ni kwa kiasi gani presha ya mchezo ilivyoathiri ufanisi wa Attackers wa Simba. Mashuti mengi ya Miquissone yalikuwa Off Target. Hii sio kawaida yake. Presha ilikuwa kubwa sana.

6: Kama kuna kitu Uongozi wa Simba unatakiwa uondoke na home work kuelekea kwenye usajili wao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa, basi ni yule kitasa wa Kaizer, ERIC MATHOHO. Ujasiri wake umeisaidia sana Kaizer muda ambao wenzake walishakata tamaa

7: Kennedy Wilson🙌 WOW. Ujio wake ulipunguza madhara ya Kaizer kwenye Aerial Ball.Alishinda mipira mingi kwenye kichwa cha Nurkovic, hii ikamfanya kocha wa Kaizer afikirie Plan B ambayo hakuwa nayo.

8: Chama 🙌 What A Player.. Hakuwa na mambo mengi leo. Aliutembeza mpira kwenye njia yake kwa kasi sana. Finishing yake ilikuwa superb sana

9: Bocco kaweka kamba 2 muhimu Lakini naamini kwenye moyo wake ataziota zaidi nafasi alizokosa kuliko alizofunga

10: Asante Tshabalala. Alikuwa superb sana kwenye kuipandisha timu na kudumbukia vyema katikati muda ambao viungo wake walivamia zone ya Kaizer

Nb: Kwa pira lile, yule dereva aandaliwe mapema 😀


No comments

Powered by Blogger.