Wasanii Kuweka Maudhui Youtube Bila Kulipa Ada ya Leseni TCRA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wamekubaliana kubadilisha Kanuni ili wasanii na wenye maudhui ambayo sio Habari waweze kurusha kazi bila kufanya usajili na malipo kwa TCRA
Hayo yamebainishwa na Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ambapo amesema kuna tofauti kubwa sana kati ya Habari na Sanaa, hivyo wataboresha kanuni
Amesema wasanii wanapaswa kufanya kazi zao bure, na kuanzia sasa wasanii wa muziki au filamu hawatalipia chaneli zao za YouTube
No comments