Wanafunzi wa shule za sekondari Kenya walala uwanjani lockdown ya Corona
Wanafunzi waliomalizi kidato cha nne wamelala katika viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi baada ya kukamilisha mitihani yao ya mwisho.
Hii ni baada ya kushindwa kuendelea na safari yao ya kuelekea nyumbani baada ya muda wa amri ya kutotoka nje kuwapata wakiwa bado hawajaondoka mjini humo kuelekea makwao.
Rais Uhuru Kenyatta alitangaza amri ya kukaa nyumbani katika kaunti 5 ukiwemo mji wa Nairobi ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Amri hiyo inatekelezwa ikiambatana na amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri.
Vituo vya habari nchini humo vimekua vikitopa taarifa kuhusu namna wanafunzi hao walivyohangaika kupata usafiri na jinsi amri ya kutotoka nje ilivyoathiri usafiri na shughuli mbalimbali mjini Naiirobi .
No comments