Simulizi ya Kuogofya ya Mwanamke Aliyemchoma Moto Mpenzi Wake
Piga picha umelala na mpenzi wako ukiwa umemuegemea, ambaye kabla ya kulala mlikuwa na furaha tu na ghafla unaamka na kujikuta umeungua.
Hii ndio simulizi ya Elvis Chidinma Omah, mtaalamu wa madawa huko mjini Makurdi, katika jimbo la Benue , katikati magharibi mwa Nigeria.
Elvis Chidinma Omah na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 17-wamekuwa katika mahusiano ya mapenzi kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kila siku penzi lao lilikuwa linakuwa na walihaidiana kuishi pamoja milele, walihaidiana kuoana na kifo ndicho kitakachowatenganisha.
Lakini msichana alianza kukosa matumaini hayo baada ya rafiki yake kumwambia amemuona mchumba wake akipeleka zawadi za harusi kwa msichana mwingine kijijini.
Ingawa Omah alikanusha madai hayo , ila mpenzi wake hakuwa ameridhika na maelezo yake na lengo lake likawa ni kuvunja uhusiano wao kwa kuchoma moto nyumba.
Omah alimpenda msichana huyo aliyemchoma moto kwa kipindi kinachokaribia miaka mitatu.
Msichana huyo aliwaambia polisi kuwa mwanaume huyo alimpa ahadi nyingi ikiwemo ya kumuoa, na kila kila kitu kilikuwa kinaendelea vizuri mara ghafla mwanaume akaanza kubadilisha mawazo.
Alipopata ujauzito wake, anasema Chidinma Omah alianza kubadilika na kuanza kufuatilia wasichana wengine.
Kwasababu ya mapenzi yake na nia ya kumuoa, alijitoa kwa kila kitu.
Baadae akamwambia atoe mimba, akatoa ya kwanza na ya pili alivyoambiwa atoe tena alikasirika sana kuwa wamepoteza mtoto mwingine.
Msichana huyo alikuwa anaanza masomo ya chuo kikuu, wakati alipoombwa na Omah alipomuomba mahusiano yao yawe kama awali.
Alikataa kwenda kwa mwanaume huyo lakini alivyoombwa sana kwenda kumuona, alienda na dumu la mafuta ya petroli na kibiriti siku ya Jumapili na kuficha katika mlango wa nyumba ya Omah.
Msichana huyo alipofika alipika chakula kitamu na hakuonesha dalili zozote za kuchukizwa na jambo lolote.Msichana aliwaambia waandishi kuwa alisubiri apate usingizi na ilipofika majira ya saa nane usiku siku ya Jumatatu, Januari 11, 2021, alichukua petroli a kumimina kwenye chumba chake na kukimbilia kanisani.
Omah aliamka na kupiga kelele, baadh ya majirani wanaume walimkimbiza hospitali .
Msichana huyo sasa yuko chini ya ulinzi na atapelekwa mahakamani baada ya uchunguzi.
Wiki za hivi karibuni , matukio ya wapenzi kuchomana moto yanaongezeka katika jimbo la Benue.
Nicodemus Nomwange, 40, alijichoma moto yeye na mpenzi wake Shiminenge Pam , na mwanamke mwingine alimchoma moto mpenzi wake huko Gboko.
No comments