Simba na Vunjabei wasaini mkataba wa Bilioni 2 kwaajili ya jezi
Klabu ya @simbasctanzania yaingia mkataba wa Bilioni mbili na Vunja Bei kwaajili ya kufanya biashara ya kuuza jezi ya timu hiyo. Vunja Bei sasa watakuwa rasmi wauzaji wa jezi kwa timu zake zote. Miwani, Kasha za Simu, Kofia, Jezi na bidhaa nyingine nyingi zenye nembo ya Simba SC zitaanza kutengenezwa na Vunja Bei na kuuzwa rasmi kwa kupitia mkataba huo mnono wa Bilioni Mbili.
No comments