Saido, Kocha Mpya Yanga Wakaa Kikao Maalum
Kocha mpya wa Klabu ya Yanga Sc, Nasreddine Nabi amezungumza na mchezaji Saido Ntibazonkiza mara baada ya mchezo wao dhidi ya Gwambina FC, hata hivyo kwa mujibu wa Afisa Habari wa Young African Hassan Bumbuli amesema kuwa mwalimu huyo hakutaka kuweka wazi juu ya kile kilichozungumzwa kwenye kikao cha na kudai mambo ya timu yanabaki huko.
Bumbuli ameyasema hayo kupitia kipindi cha Sports Arena cha Wasafi Radio ”Mwalimu alimuita Saido na kuzungumza naye, wamezungumza mambo mengi kama dakika 15, 20 hivi walikuwa wamekaa wanazungumza.”- Hassan Bumbuli Afisa Habari wa Yanga SC.
”Mwalimu hakutaka kuweka wazi lakini mimi binafsi aliniambia kuna mambo yakitokea lazima mwalimu azungumze na wachezaji, kwahiyo hakutaka kuweka wazi, amesema mambo ya kwenye timu yanabaki kwenye timu.”- Bumbuli.
Hata hivyo Kocha huyo ataendelea kusalia kama mshauri tu mpaka pale taratibu zote zitakapokamilika za kukabidhiwa timu kutoka katika mikono ya Mtanzania Juma Mwambusi.
No comments