Header Ads

Header ADS

RC Mghwira: Idadi ya waliofariki ajali iliyohusisha magari mawili Same yafika 11

 
Idadi ya watu waliofariki katika ajali iliyohusisha magari mawili wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro imefikia 11 baada ya mmoja kati ya majeruhi wanne waliofikishwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC kufariki Dunia wakati akipatiwa matibabu.

Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Dkt Anna Mghwira amefika katika hospitali ya Rufaa ya KCMC kuwajulia hali majeruhi wengine wa ajali hiyo iliyohusisha magari mawili , Toyota Alphard (T 898 DKX )na Toyota Hiace (T 806 BNM)


No comments

Powered by Blogger.