Presha ya Ubingwa ni kubwa sana – Haruna Niyonzima
Kiungo Fundi wa soka kutoka kwa Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amesema kuwa kwa upande wake presha ya Ubingwa ya mwaka huu anaiyona ni kubwa mno na kwasababu tangu aanze soka lake la kulipwa hapa nchini Yanga haijawahi kukosa Ubingwa huo wa Vpl mara tatu mfululizo.
Niyonzima ameyasema hayo hii leo wakati wakijiandaa kuwakabili Gwambina FC hapo kesho siku ya Jumanne ”Tumejiandaa vizuri, kama alivyosema mwalimu, mchezo wa kesho utakuwa mchezo mgumu, kwasababu naamini Gwambina FC wametoka kupoteza mchezo juzi so sidhani kama watakubali kupoteza mchezo unaokuja wa kesho.”
Niyonzima ameongeza ”Sisi kama Yanga, bila shaka nimesema kila mechi tunahitaji kushinda, hivyo tumejiandaa vizuri na mimi naamini kwa uwezo wa Mungu mechi kesho itakuwa nzuri kwa upande wetu.”
Kuhusu presha ya Ubingwa mwaka huu ”Presha ni sehemu ya mpira wa miguu, lakini naweza kusema presha ya mwaka huu ni kubwa sana kwasababu pia, tangu nije Tanzania Yanga haijawahi kukosa Ubingwa mara tatu mfululizo kama ilivyokuwa sasa hivi na naweza kusema hicho ndiyo kitu ambacho kimeweza kuchangia presha ya sasa hivi.”
”Kwangu mimi sijawahi kupata presha hiyo lakini bila shaka presha ipo siku zote ila ni jambo la kawaida kwenye mpira na mimi napenda kuwaambia wachezaji, mchezaji yoyote asiyekubali presha ni bora aache mpira.”
No comments