Header Ads

Header ADS

"Nilijiangalia Nikaona Ufupi Huu Sitoboi"- Ebitoke


Unakumbuka Mchekeshaji Ebitoke alipotangaza kugombea kushiriki shindano la Miss Tanzania 2020, sasa msanii huyo amefunguka kusema shindano hilo lilimshinda kwani alijiangalia kwenye kioo akasema kwa ufupi alionao asingeweza kushinda.

Akizungumza na eNewz ya East Africa TV inayoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12:00 Jioni, Ebitoke amesema


"U-Miss ulinishinda kwa sababu nilijiangalia kwenye kioo mara nyingi nikasema na ufupi huu nitaenda kuwa miss gani 'high hills' zenyewe kutembelea shida,  kiukweli nina kasura fulani hivi ila umiss ulinishinda na sio fani yangu" amesema Ebitoke



No comments

Powered by Blogger.