Mimba ya mama Yadaiwa Kuyeyuka
KUMEKUCHA! Imebainika kuwa mimba ambayo Mama mzazi wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika na bosi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’, aliyodaiwa kuwa anayo, imeyeyuka.
AMANI linakupakulia uhondo.Ukweli huo umeanikwa na chanzo cha karibu ambacho kimedhibitisha kuwa mama huyo hakuwa mjamzito kama ilivyokuwa imevumishwa hapo awali.
“Nimezungumza naye ana kwa ana, pia nimemuangalia kwa makini tumbo lake kwa sababu yule ni shoga yangu kabisa, kaniambia hana mimba. Alikuwa anawazuga tu watu wambeya.“Aliniambia… ‘shoga yangu, mimi nibebe mimba na uzee huu, ninatafuta nini… hebu niacheni bana, siwezi kubeba mimba nikafie leba bure.’
Ndivyo alivyokanusha Mama Mondi,“ kilieleza chanzo chetu.Taarifa za mama Diamond kudaiwa kuwa ni mjamzito zilianza kuibuka mara baada ya kuvuja kwa video inayomuonesha bi mkubwa huyo akiwa kwenye viti vya uwanja wa ndege, akitaka kusafiri na kuonekana kama anaziba tumbo lake kwa kutumia pochi yake.
Kama hiyo haitoshi, ilivuja video nyingine siku ya Sikukuu ya Pasaka ambayo ilimuonesha mama Diamond akiwa na ‘chawa’ kama wote ndani ya boti wakisherehekea lakini mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’ alisikika akiinadi mimba ya Bi Sandra.
“Mmemuona baby wetu…baby wetu…baba mtoto mnamuona…mnamuona….baba mtoto mnamuona?” alisikika Dida huku video hiyo ikionesha kwa ukaribu tumbo la mama Diamond lililojaajaa pamoja na Maisara Abdul maarufu kama Uncle Shamte.
Hii si mara ya kwanza Mama Mondi kukanusha madai hayo ya mimba kwani Novemba mwaka jana, Mama Mondi aliwajibu wanaomtaka amzalie mtoto mumewe, Uncle Shamte.
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, Mama Dangote alimjibu shabiki mmoja aliyemuuliza mbona habebi mimba? Mama huyo mwenye zaidi ya umri wa miaka 50 alimjibu; “Siko kwenye kubeba mimba, mimi ni bata kwa kwenda mbele!’’
STORI:MWANDISHI WETU, DAR
No comments