Makonda Afunguka 'Sio Lazima Kuteuliwa'
ALIYEKUWA mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwa sasa sio lazima ateuliwe au apigiwe kura kuwa kiongozi, anaweza kuongoza hata familia yake.
Ameyasema hayo jana Jumanne Aprili 20, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahafali ya kuhitimu stashahada ya uzamili ya uongozi katika Chuo Kikuu cha Aalto cha Finland kikishirikiana na Taasisi ya Uongozi Tanzania.
“Mimi ni mkulima, ni mfanyabiashara pia kwa hiyo ninaweza kuwa na mchango mkubwa sana hata kwenye kampuni ninazoweza kufanya kazi. Siyo lazima uwe kiongozi wa kuteuliwa au wa kupigiwa kura, unaweza kuwa kiongozi hata wa familia,” amesema Makonda.
No comments