Header Ads

Header ADS

Kocha Mbrazil Amzuia Manula Kuondoka Simba





KOCHA wa makipa wa Simba, Mbrazil, Milton Nienov amefichua kuwa ni suala gumu kukubali kuondoka kwa kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula kwa kuwa timu hiyo bado ina mipango naye ya muda mrefu.

 

Kocha huyo ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa tetesi za kipa huyo kutakiwa na Klabu ya Al Merrikh ya Sudan ambayo imetangaza dau la sh milioni 230 na mshahara wa Sh milioni 18 kabla ya Mamelodi Sundowns kumtangazia dau la sh milioni 500.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Nienov alisema kuwa ni suala gumu kwa sasa kwa Simba kukubalia kumuachia kipa huyo kwa kuwa bado wana malengo naye katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

 

“Sijui nikwambie kitu gani kwa sababu sina taarifa zozote juu ya hilo lakini naamini bado litakuwa ni jambo gumu kwa sababu Simba bado inamuhitaji zaidi hasa katika hii michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

 

“Haliwezi kuwa jambo rahisi kwa klabu kuweza kukubali kumuachia mmoja kati ya makipa wake bora hasa katika kipindi ambacho timu ipo kwenye mashindano makubwa, naamini ni jambo ambalo haliwezi kukubalika kwa sababu timu bado inamuhitaji kutokana na rekodi yake katika michuano husika,” alisema Nienov.




No comments

Powered by Blogger.