Kamanda Mambosasa Afafanua Sakata la Kukamatwa Kajala na Paula
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa msanii wa filamu, Kajala Masanja na mwanaye Paula na kueleza kwamba walikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kwa tuhuma za kudaiwa kusambaza picha chafu mitandaoni.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Kamanda Mambosasa amesema Kajala na mwanaye Paula walikamatwa alfajiri ya Jumanne, April 20,2021 kwa ajili ya mahojiano na wakaachiwa siku hiyohiyo, majira ya saa moja jioni.
Ameongeza kuwa wawili hao wataendelea kuripoti polisi mpaka hapo jalada la upelelezi wa kesi yao litakapokamilika na kufikishwa mahakamani kwa kuwa kesi za aina hiyo huchukua muda mrefu kuzifanyia uchunguzi.
Kajala na Paula wanatuhumiwa kusambaza picha chafu mitandaoni zinazodaiwa kuwa ni za msanii wa Bongofleva, Abdul Kahali ‘Harmonize’.
No comments