Fahamu kuhusu Kimbunga Jobo kinachotarajiwa kuikumba Tanzania
Baada ya kutangazwa ujio wa kimbunga Jobo kwenye Pwani ya Afrika Mashariki hada Dar Es Salaam, Tanga, Zanzibar, Mtwara na Lindi.
Vyombo mbalimbali vya Habari vya Kimataifa ikiwemo Aljazeera na CNN vimeripoti kuwa kuna uwezekano wa Kimbunga Jobo kuikumba Tanzania Weekend hii.
Iwapo Kimbunga kitatokea haitokua mara ya kwanza kwa Tanzania kukumbwa na kimbunga kwani historia inaonesha kiliwahi kutokea kimbunga kingine kwenye karne ya 19.
Kimbunga cha kwanza kiliikumba Zanzibar mwaka 1872 na miaka 80 baadaye Kimbunga kingine kiliikumba Lindi mwaka 1952.
Lakini pia wakieleza kitaandamana na mvua kubwa na upepo. Watanzania wanaoishi maeneo tajwa wanaombwa kuchukua tahadhari mapema kabla ya kukumbwa na kimbunga hicho.
No comments