Header Ads

Header ADS

Rayvann Amuomba Msamaha Kajala




MSANII Raymond Shaban Mwakyusa aka Rayvanny aliye chini ya label ya Wasafi Classic Baby (WCB) kupitia ukurasa wake wa Instagram amemwomba msamaha muigizaji Kajala Masanja ambaye ni mama mzazi wa  Paula Masanja.

“Duniani wakati mwingine kuna vitu tunavifanya ambavyo pengine kwa macho yetu ya ujana tunaona ni sahihi lakini tunasahau upande mwingine wa pili ambao ni wazazi wanaoumia kwa namna moja au nyingine. Nichukue nafasi hii kumuomba radhi dada angu Kajala Masanja na kuwaomba radhi wazazi na yeyote ambaye nilimkwaza kwa kupost video ambayo inawezekana imetafsiriwa vibaya …kwa sababu sisi ni binadamu na kamwe hatuwezi kukamilika” alisema Rayvanny.






No comments

Powered by Blogger.