Ukweli usemwe: Nandy ni Msanii Namba Moja wa Kike Ambaye Tumebarikiwa kwa sasa
Kama mnakumbuka ujio wa Nandy alianza baada ya Ruby kukorofishana na Clouds media. Watu wengi nikiwapo mimi walikuwa wana doubt sana kipaji cha Nandy toka awali.. na kama kipindi kile watu walikuwa wakimsikia Nandy basi utawasikia wakisema hamna kitu huyo ameletwa kumfunika Ruby lakini hana kipaji kabisa.
Lakini kwa Msanii Nandy ilikuwa tofauti kwani kila wakati ukipata kusikiliza wimbo wake unagundua kabisa hapa tunaye msanii wakike hodari kabisa.
Msanii Nandy ni bora sana kwenye vitu vingi ukilinganisha na wasanii wenzie wakike kwa sasa.
Ukisikiliza wimbo wa Nandy wa sasa utaona utofauti kabisa na wimbo wa juzi na jana na hiki ndicho kinawashinda wasanii wengi wa kike kwa sasa maana wengi wao karibu nyimbo zote zinafanana kabisa kila kitu.
Pia swala la utulivu kwenye stage linamfanya Nandy awe bora sana kuliko wasanii wenzie wa kike... wasanii wakike wanatatizo la uwezo wa kusikika wakiwa kwenye jukwaaa, wengi wao wanapiga kelele sana tena sana hadi unaweza kujiuliza kama ndio huyu unayemsikia kwenye radio au lah.
Ukimsikiliza Nandy unaona kabisa kipaji kikubwa sana ambacho kinajua kutumiwa vilivyo tofauti kabisa na wasanii wetu wa kike natamani sana kama Rubby angeliamka usingizini akapambana maana ni Rubby pekee ndio ana uwezo mkubwa lakini amelala na aambiliki na ndiye msanii anayefanya Nandy aendelee kutamba kwa Level yake.
No comments