Tyrese Afunguka Kuhusu Tik Tok "Watu Wazima Mnaonekana Kama Vichaa Kwa Ajili ya Views"
Mwimbaji na Muigizaji wa Marekani Tyrese ameibuka na mapendekezo kwa ajili ya mtandao wa TikTok, amesema inabidi waweke kigezo cha ukomo wa umri kwani watu wazima waliopo kwenye mtandao huo wanaonekana kama vichaa, yote kwa ajili ya kupata views tu
"Naweza kulisemea hili kwa sababu linatakiwa kusemwa. TikTok wanabidi kuweka ukomo wa umri. Baadhi yenu ninyi watu wazima huku mnaonekana kama vichaa kwa ajili ya views, wakati watoto wenu wenye miaka 9 wakiwa nyumbani wanabaki kusema 'Mama/Baba mnapandisha videos kila siku, mnacheza huku mkionekana kama vichaa na mnaishia kutopika chakula cha usiku kwa wiki 3." aliandika Tyrese na kumalizia
"Facebook, Instagram, Twitter, huu upuuzi wote ni kwa ajili ya watoto." ulisomeka ujumbe wa Tyrese ambao tayari ameufuta hapa instagram.
No comments