Tabu Mitimingi "Kibenten Wangu Nimempata Kwa Elfu 30 tu"
MC na msanii wa filamu Tabu Mtingita ameweka wazi kuhusu mahusiano yake na mpenzi wake Lexy Gitaa ambaye amemzidi umri kwa kusema alimpata kwa shilingi Elfu 30 tu, baada ya kutaka kumtangazia biashara yake ya mapochi.
Mc Tabu Mtingita amesema yeye na mpenzi wake huyo wamedumu kwa muda wa miaka mitano na kikubwa anachomvutia ni unene alionao.
"Mpenzi wangu sio maarufu na kama umaarufu ataupata kupitia mimi, tupo kwa miaka mitano na nimetambulishwa mpaka ukweni, amependea unene wangu alikuwa ananilipa Elfu 30 kwa tangazo moja, na pesa ile ilikuwa na faida kwangu kwani ndiyo imefanya nimpate" amesema Tabu Mtingita
No comments