Rubani wa Jeshi la Uganda afarika katika ajali ya helikopta
Jeshi la Uganda limethibitisha kifo cha rubani wa helikopta iliyoanguka muda mfupi tu baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe siku ya Alhamisi.
Msemaji wa jeshi la Uganda UPDF) Brigadia Flavia Byekwaso amesema tukio hilo lilitokea wakati wa kupindi cha mafunzo ya uendeshaji wa ndege.
"TLeo mchana majira ya saa nane na robo ndege aina ya jet iliyokuwa ikiendeshwa na marubani wawili wanafunzi wa mafunzo ya kijeshi ya cadet ilianguka mara moja baada ya kuondoka karibu na ufukwe wa Lido (Lido beach). Wawili ao walikimbizwa hospitalini kuchunguzwa afya zao ," alisema.
Marehemu alitambuliwa kama Kapteni Caroline Busingye.
No comments