Janjaro Afunguka Kutekwa na Mapenzi na Kuhama DSM
Msanii kutoka lebo ya MMB chini ya Madee Seneda, Dogo Janja amefunguka kusema ni kweli anayapenda mapenzi lakini sio kama amehama Jijini Dar Es Salaam na kwenda kuishi Arusha kwa mpenzi wake Quenlinna Totoo.
Dogo Janja amesema huonekana mara chache sana kwenye shughuli maalum ndiyo maana watu wanadai kama amehama kumfuata mpenzi wake
"Dar Es Salaam nipo sana ila huwezi jua nilipo, nitatokea kukiwa na ishu muhimu maana sipendi kuonekana hovyo lakini watu wangu wa mtaani wananiona kila siku, mapenzi hayajawahi kuniteka ila nayapenda na nikipenda huwa nipo karibu na mpenzi" amesema Dogo Janja
No comments