Gigy Money Amshukuru Mungu Kwa Kubadilika
MSANII wa muziki Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu ‘Gigy Money’ amesema anamshukuru Mungu kwa sasa amebadilika, anaishi kistarabu kadiri alivyokuwa anapaswa kuwa.
Amesema mabadiliko hayo ni kutojibizana na watu kitu ambacho siku za nyuma alikuwa akikifanya sana.
“Taratibu naanza kuwa niliyetakiwa kuwa muda mrefu, sina marafiki wengi, sijibizani tena na watu, nainjoi upweke wa hapa na pale, naridhika na vichache nilivyobarikiwa, sibembelezi ukaribu na mtu,” alisema Gigy Money ambaye kwa sasa anatumikia adhabu kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ya kutojihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa muda wa miezi sita.
Adhabu hii ni baada ya mkali huyo akiwa katika Tamasha la Wasafi Media, Tumewasha Tour lililofanyika jijini Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri, kupanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza akiwa ametinga vazi ambalo lilikuwa linaonyesha maungo yake ya mwi
No comments