Header Ads

Header ADS

Wachezaji 4, Rais, Rubani Wafariki kwa Ajali ya Ndege Brazil





WACHEZAJI wanne akiwemo rais wa klabu ya soka ya Palmas, Brazil, na rubani wamefariki katika ajali ya ndege ndogo jana, Jumapili.

 

Waliofariki ni Ranule (golikipa), Lucas Praxedes (mlinzi), Guilherme Noe (mlinzi). Marcus Molinari (kiungo), Lucas Meira (rais) na ruban aliyejulikana kwa jina moja la Wagner.

 

Ndege hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa Tocantinense karibu na jiji la Palmas wakati ikielekea Goiania, kilomita 800 kutoka Palmas ambapo klabu hiyo ilikuwa icheze mechi leo (Jumatatu).

 

 



 

Mwaka 2016,  kikosi kizima cha klabu ya Chapecoense kikiwa na watu 71 kiliangamia wakati ndege iliyokuwa inawapeleka katika fainali ya mashindano ya Copa Sudamericana huko Colombia ilianguka mlimani nje ya Jiji la Medellin.  Miaka miwili baadaye Fernandao,  nahodha wa klabu ya Internacional alifariki wakati  helikopta yake ilipoanguka katika jimbo la Goias.

 




No comments

Powered by Blogger.