Virusi vya Corona Uingereza ni hatari zaidi – Waziri Mkuu Boris Johnson
Utafiti wa awali unaonesha kuwa virusi vipya vya ugonjwa wa corona vilivyojitokeza Uingereza ndio hatari zaidi, amesema Waziri mkuu Boris Johnson.
Data hiyo imetokana na kulinganishwa kwa idadi ya vifo kati ya watu waliopata maambukizi na virusi vipya ama vile vya zamani vya corona.
Maambukizi yanayosababishwa na virusi vipya tayari yamesambaa kote Uingereza.
Bwana Johnson amesema katika taarifa: “Mbali na kwamba vinasambaa kwa haraka, sasa hivi pia inaonekana kana kwamba kuna ushahidi kuwa virusi vipya – vile ambavyo mara ya kwanza kabisa vimebaini London na kusini mashariki – huenda vikahusishwa na idadi ya juu ya vifo.
“Yaani athari kubwa imetokana na virusi hivyo vipya na hilo linamaanisha wizara ya afya sasa hivi inakumbana na shinikizo kubwa.”
Kundi lililokuwa linafanya utafiti, limehitimisha kuwa “kuna uwezekano mkubwa” virusi hivyo vimekuwa hatari mno.
Alisema: “Nataka kusisitiza kuwa bado kuna sintofahamu kuhusiana na idadi na juhudi zaidi zinahitajika lakini bila shaka inatia wasiwasi kwamba virusi hivyo vimechangia ongezeko la idadi ya vifo pamoja na kiwango chake cha maambukizi.”
Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa virusi vipya vinasambaa kwa asilimia 30 na 70 haraka zaidi ya virusi vyingine na inasemekana kuwa ni hatari zaidi kwa asilimia 30. Virusi hivyo vipya mara ya kwanza vimebainika Kent mnamo mwezi Septemba. Na sasa hivi vinapatikana kwa nchi zaidi ya 50 maeneo ya England na Ireland Kaskazini.
Chanjo za kampuni ya Pfizer na ile ya AstraZeneca ya Oxford – zote zinatarajiwa kuwa na ufanisi dhidi ya virusi hivyo vipya ambavyo vimejitokeza nchini Uingereza.
Hata hivyo, Sir Patrick, mshauri mkuu wa serikali juu ya masuala ya sayansi, amesema kuna wasiwasi kuhusu virusi vingine viwili ambavyo vimejitokeza Afrika Kusini na Brazil.
“Kwa sasa, hivyo ndio vyenye kutia wasiwasi zaidi ikilinganishwa na vile vya Uingereza na tunachohitajika kufanya ni kuvifuatilia na kuvichunguza kwa makini.”
Waziri mkuu alisema serikali ya Uingereza imejitayarisha kuchukua hatua zaidi kulinda mipaka ya nchi hiyo kuzuia virusi hivyo vipya kuingia nchini humo.
“Siondoi uwezekano wa kuchukua hatua zaidi,” alisema.
Wiki iliyopita serikali ya Uingereza ilipiga marufuku nchi ya Amerika Kusini, Ureno na nchi nyingi za Afrika huku wasiwasi juu ya virusi hivyo vipya ukiendelea kuongezeka.A computer-generated graphic of the virus in front of red blood cells
Je virusi hivi vipya ni vipi?
Wasiwasi wa wataalamu sasa hivi umejikita katika aina chache ya virusi vipya vya maambukizi ya corona:
Virusi vya Uingereza vimeenea sana Uingereza na kusambaa kwa zaidi ya nchi zingine 50.
Virusi vya Afrika Kusini ambavyo pia vimepatikana katika nchi zisizopungua 20 ikiwemo Uingereza.
Virusi vya Brazil.
Sio ajabu kwamba kumejitokeza virusi vipya kwasababu virusi vyote hujibadilisha wakati vinaendelea kuzaliana ili kusambaa na kuendeleza uwepo wao zaidi
Sasa hivi kuna maelfu ya virusi vipya vya corona vinavyosambaa.
Je virusi hivyo ni hatari kiasi gani?
Inashukiwa kuwa virusi vya Uingereza, Afrika Kusini na Brazil huenda ndio vinavyoambukiza zaidi au vilivyorahisi mtu kuvipata kuliko vile vya awali.
Vitusi vyote hivyo protini yake imebadilika- ikiwa ni sehemu ya virusi yenye kuhusishwa na seli za binadamu.
Matokeo yake, virusi hivyo vinaonekana kuwa na uwezo wa juu wa kuambukiza seli na kusambaa.
Je chanjo bado itafanyakazi?
Chanjo za kwanza zimetengenezwa kwa kuzingatia virusi vya awali vya corona lakini wanasayansi wanaimani kwamba bado chanjo zitafanyakazi ingawa pengine huenda zisiwe na ufanisi mkubwa.
Utafiti unaendelea ikiwa ni pamoja na kufuatilia kile kinachoendelea katika maisha halisi watu wanapopata chanjo.
Chanjo inafanya mwili kuzoea kushambulia sehemu mbalimbali za virusi hata hivyo, sio tu hayo pekee.
Huenda vurusi vipya vikajitokeza siku za usoni ambavyo ni tofauti kabisa.
Hata hali ikiwa mbaya zaidi, chanjo hizo huenda zikaboreshwa tena katika kipindi cha wiki kadhaa au hata miezi ikiwa kutakuwa na haja ya kufanya hivyo, wamesema wataalamu.
Kama ilivyo kwa chanjo za mafua, ambapo kila chanjo mpya hutolewa kila mwaka kukabiliana na mabadiliko yoyote katika usambaaji wa virusi vya mafua, huenda kukawa na kitu kama hicho kwa virusi vya corona.
No comments