Header Ads

Header ADS

TANZIA: Msanii wa Bongofleva C Pwaa afariki Dunia



Msanii wa Bongofleva Ilunga Khalifa maarufu C Pwaa amefariki Dunia Alfajiri ya leo akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa Ndugu wa karibu wa C Pwaa amethibitisha kuwa Pwaa alikuwa anaugua Pneumonia na alifikishwa Hospitali kwa matibabu, hali yake haikuwa njema hadi umauti unamkuta.


Enzi za uhai wake C Pwaa alifanya vizuri akiwa na kundi la Park Lane pamoja na Suma Lee ambapo walitoa ngoma kama Nafasi Nyingine na Aisha, na baadaye alitoa ngoma zake nje ya kundi zikiwemo Action, Problem, So Pwaa, Six in the Morning nk.



No comments

Powered by Blogger.