Rais Weah ‘Amkataa’ Cristiano Ronaldo
Mchezaji wa zamani wa AC Milan, George Weah amesema Cristiano Ronaldo sio mchezaji bora ulimwenguni, lakini anamchukulia mreno huyo kama kioo kwa wachezaji wachanga.
“Namfananisha Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic ambaye kwa sasa wachezaji chipukizi wengi wanajifunza kutoka kwake licha ya umri kumtupa mkono lakini bado anasakata kabumbu kwa kiwango kikubwa“ amesema Weah amabaye pia kwa sasa ni Rais wa nchi ya Liberia.
Weah anaamini Ronaldo kutokana na kujituma kwake bado ataendelea kutikisa katika ulimwengu wa soka hata kama akifikisha umri wa miaka 40.
No comments