Rais Magufuli Awapa Siku 7 Waziri Gwajima na Jafo, Kisa Hichi Hapa
Rais Dkt John Magufuli, amewapa siku 7 Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, kuhakikisha wanaweka usawa katika suala la ugawaji wa madawa kwa mkoa wa Geita, kwani licha ya kwamba bajeti ya dawa imeongezeka lakini mkoa huo umekuwa ukipata dawa chache.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 27, 2021, wakati akizindua majengo ya kituo cha afya cha Masumbwe, na ndipo alipobaini changamoto ya upunjwanji wa mgao wa madawa, licha ya kwamba bajeti ya madawa imeongezeka, hali aliyopelekea kutoa maagizo haya.
"Inawezekana kuna upunjaji wa mgawo wa madawa katika maeneo ya mkoa huu ikiwepo Masumbwe, bajeti ya madawa imeongezeka lakini dawa zinazotolewa katika mkoa huu ni chache, Waziri wa Afya na Waziri TAMISEMI mnaopanga bajeti ya madawa mkakae ndani ya siku 7 mje na majibu ni kwa namna gani madawa yataongezeka katika hospitali ya Masumbwe na maeneo mengine", amesema Rais Dkt. Magufuli.
Join Our Telegram Group for Job Updates CLICK HERE
Aidha Rais Magufuli pia aligusia suala la idadi ya watumishi wa afya katika Hospitali hiyo ya Masumbwe, na kuacha maagizo kwa Wizara ya Afya na TAMISEMI na kuzitaka ziwe na ushirikiano ili mambo yaende vizuri.
No comments