Header Ads

Header ADS

NIGERIA; Wasichana waliotekwa na Boko haramu mwaka 2014 wafanikiwa kutoroka (+ Video)

 


Taarifa kutoka Nigeria zinasema kwamba wasichana zaidi waliokuwa wametekwa nyara kutoka shule ya wasichana Chibok mwaka 2014 wametoroka kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram. Baba wa mmoja wa wanafunzi wa zamani wa Chibok ameiambia BBC kuwa alizungumza na binti yake ambaye amenusurika.

Amesema walizungumza nae kwa njia ya simu baada ya kufanikiwa kutoroka na alikuwa analia.

Yeye na wasichana wengine waliotekwa nyara katika shule ya wasichana ya Chibok na maeneo mengine wameripotiwa kutoroka kutokana na operesheni za kijeshi dhidi za jeshi la Nigeria dhidi ya Boko Haram.



No comments

Powered by Blogger.