Header Ads

Header ADS

Makaburi yagundulika katika eneo la vitu vya kale Misri



Wanaakiolojia wametoa taarifa zaidi juu ya umuhimu wa eneo la makaburi lililogulika la Saqqara, katika eneo la kale la Misri, kusini mwa mji mkuu wa Cairo.

Taarifa za ugunduzi wa makaburi hayo zilijitokeza Jumamosi, na wataalamu wamekuwa wakilizungumzia suala hilo la makaburi 50 yaliyogunduliwa.


Moja ya makaburi hayo lilikuwa ni la mwanajeshi ambaye alikuwa amezikwa na silaha yake ya shoka.


Vifaa vingine vilivyopatikana ndani ya makaburi hayo ni pamoja na barakoa, mashua na vilikuwa vimeandikwa maneno kutoka kwa kile kilichosemekana kuwa "kitabu cha wafu".


Michezo waliopenda watu wa kale wa Misri ilikuwa imewekwa kwenye miili ya wafu ili waweze kuicheza katika maisha ya baada ya uhai.


Mwanaakiolojia mkuu alisema inaaminika kwamba walioshinda mchezo unaojulikana kama "Senet" watapita mtihani na kuingia peponi.



No comments

Powered by Blogger.