Header Ads

Header ADS

Maelfu Wazuiwa Guatemala Kuingia Marekani





MSAFARA wa wahamiaji kutoka Amerika Kusini uliokuwa ukielekea nchini Marekani umekutana na virungu na gesi za kutoa machozi nchini Guatemala, ambako vikosi vya usalama vilifunga njia yao ya kupita kuelekea Marekani.

 

Maelfu ya watu walizuiwa kwenye barabara karibu na mpaka wa Guatemala na Honduras, ambako serikali  nchini humo imesema msafara huo ulivunja sheria za nchi hiyo.

 

Wahamiaji wanaokadiriwa kuwa 7,000 wengi wao kutoka Honduras, wameingia Guatemala  katika siku za hivi karibuni, wakikimbia umasikini na ghasia, lengo lao ikiwa ni kusafiri hadi Mexico, na baadaye kuufikia mpaka wa Marekani.



Kila mwaka, maelfu ya wahamiaji wa Amerika ya Kati hujaribu  kufika Marekani, mara nyingi, kwa hutembea kwa miguu.

 

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden, kutoka chama cha Democrat, ameapa kuondoa sera kali za uhamiaji zilizowekwa na mtangulizi wake, Donald Trump, kutoka Republican.

 

Lakini utawala wa Biden, ambao utachukua mamlaka Jumatano, umewaonya wahamiaji kutofanya safari hizo kwa sababu sera za uhamiaji hazitabadilishwa haraka.

 



No comments

Powered by Blogger.