Header Ads

Header ADS

Chriss Brown Amjibu Vibaya Shabiki Aliyelinganisha Uwezo Wake


Chris Brown hataki jina lake na uwezo wake ulinganishwe na mtu yeyote hapa duniani, amjibu kwa maneno makali shabiki mmoja ambaye alilinganisha uwezo wake na mchezaji wa NBA, Ben Simmons.


Shabiki huyo aliandika kupitia twitter kwamba Chris Brown na R&B yake ni kama Ben Simmons kwenye Kikapu. Yani hakuna maendeleo yoyote wala hatua anayopiga, hashuki, yuko vile vile, ni msanii wa hovyo tu.


Breezy alishindwa kuvizuia vidole vyake na kuamua kumshushia maneno makali shabiki huyo akitaka asimchezee hata kidogo na asimlinganishe na mtu yeyote. Kubwa zaidi alimwambia "Sasa nenda kamuulize mama yako, yupi ni baba yako halisi." 



No comments

Powered by Blogger.