Header Ads

Header ADS

Babu Tale – Marehemu Mke Wangu Aliniambia Nimechoka Kuishi, Mimi Naondoka ila Usioe




MBUNGE wa Morogoro Kusini Mashariki, Mhe. Hamisi Taletale ‘Babu Tale’, ambaye alifiwa na mkewe, Shamsa Kombo ‘Shammy’, Juni 26, 2020, amefunguka mazito kuhusiana na marehemu mke wake huyo kwenye mahojiano na mtangazaji Salama Jabir kwenye kipindi chake cha SalamaNa.



“Marehemu mke wangu tulifahamiana Magomeni Kota kwa sababu na yeye alikuwa anaishi pale, nilimtongoza mwaka mzima hajanikubali. Enzi hizo nilikuwa mtu flani rafu halafu yeye ana mambo ya Kizungu” ameeleza Babu Tale.



“Mke wangu aliniambia nisioe, nakumbuka hiyo siku nimeshinda naye Muhimbili, akaniambia nimechoka kuishi hii hali, akanishika mkono kuniambia mimi naondoka, lea watoto lakini usioe, usioe, usioe.”


BabuTale aliendelea, “Kinachoniliza ni kupoteza mtu ambaye angeweza kuniongoza kwa vitu vingine, nimepata uongozi lakini yule aliyetakiwa kula good time hayupo”.


Marehemu Shammy enzi za uhai wake alifahamika zaidi kutokana na asasi yake aliyoimiliki ya ‘Nasimama Nao‘ iliyokuwa ikiwasaidia kina mama na mpaka mauti yalipomkuta, ameacha watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.




No comments

Powered by Blogger.