Header Ads

Header ADS

Askofu Shoo amvaa meya aliyewavua watu barakoa



Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu kuwaamuru wananchi waliokuwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kuvua barakoa.


Askofu Shoo, ambaye pia ni mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo, alisema kitendo cha meya huyo kuwalazimisha wananchi wanne kuvua barakoa ni kukosa hekima na uwajibikaji wa kiwango cha juu kama kiongozi wa kisiasa.


“Itoshe tu kusema nimesikitishwa sana na kitendo cha huyu meya, kuwalazimisha watu kuvua barakoa, ni kukosa hekina na uwajibikaji kwa kiwango cha juu,” alisema Askofu Shoo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kujikinga.



No comments

Powered by Blogger.