Header Ads

Header ADS

Anaitwa Ibenge: Tetesi za usajili Simba, Yanga na Azam na klabu nyingine Bongo

 


Wakati huu ambao Simba haina kocha baada ya kuondoka Sven, kumekuwa na tetesi nyingi juu ya makocha mbalimbali kuhusishwa na kutaka kujiunga na Mabingwa hao tetezi Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

FLORENT IBENGE Amezaliwa Disemba 4, 1961 (age 59) mzaliwa wa Kinshasa, Democratic Republic of Congo


Kwa sasa Ibenge ni sehemu ya benchi la ufundi katika timu ya taifa ya DR Congo.


Lakini usisahau kwa sasa ni kocha wa Vita Club a. k. a The Black Dolphins


Alishawahi kusakata kabumbu na nafasi yake ilikuwa Defender.


Ameshawahi kuwa kocha wa klabu zifuatazo

2012- Shanghai Shenhua

2014- Vita Club

2014-2019 DR Congo

2019- Vita Club


Tetesi zilizopo kwenye sajili za soka nchini Tanzania zinadai kuwa Miamba ya soka Ligi Kuu Tanzania Bara na Mabingwa wa Nchi #simbasc wamemsaini kinda wa miaka 19 raia wa Congo kiungo wa klabu ya DC Motema Pembe, Karim Kiekie Kamvuidi.

 

Karim kwa sasa yuko Cameroun na timu ya Taifa ya Congo DR kwenye mashindano ya CHAN. Kwenye mchezo wa timu yake ya taifa na Tanzania Taifa Stars alivalia jezi namba 17.


Wakati Mnyama Simba akiwa mbioni kutafuta mbadala wa Sven, inadaiwa mabingwa hao watetezi Ligi Kuu wamefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Klabu ya Pyramids ya nchini Mirsi, Sebastian Desbare ili kuja kurithi mikoba ya Sven Vanderbroek aliyeondoka baada ya kuivusha Simba hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

 

Yanga imefanikiwa kumsajili, Fiston Abdulrazaq ambaye walimtangaza mapema mwanzoni mwa wiki hii na hawa ndiyo waliyosajiliwa mpaka sasa dirisha dogo Said Ntibazonkiza – Mshambuliaji, Fiston Abdulrazaq – Mshambuliaji na Dickson Job – Beki.



No comments

Powered by Blogger.