Timu zatahadharishwa kutoingia Uwanja wa Nelson Mandela na Matokeo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa tahadhari kwa timu za Yanga na Tanzania Prison kutoingia uwanjani na matokeo katika mchezo wao wa raundi ya pili utakaochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga siku ya Alhamisi ya tarehe 31.12.2020
Amesema kuwa timu hizo mbili zilipokutana katika raundi ya kwanza jiji Dar es Salaam hakukuwa na mbabe hali ambayo inaifanya vinara wa ligi hiyo kukamia kupata pointi tatu ugenini huku Tanzania Prison ikikataa kuwa mnyonge katika uwanja wa nyumbani na hivyo kutokubali kufungwa na kuwakumbusha kuwa mchezo una matokeo matatu na kila timu iwe tayari kuyapokea matokeo hayo.
“Wapenzi wa mpira wa miguu wafike kwa wingi waweze kujione mshindi atakuwa ni nani, kwasababu mpira una matokeo matatu, kuna kushinda, kufungwa lakini pia kuna sare, timu zote mbili zijiandae kwa matokeo hayo matatu, isije mtu anakuja na matokeo yake hapa kwamba mimi nitashinda halafu akashindwa halafu akafanya fujo, sasa sisi vyombo vya ulinzi na usalama tumeshajiweka vizuri kwa fujo zozote ambazo mtu amejiandaa nazo aziache huko huko,” Alisisitiza.
Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokwenda kuutembelea Uwanja wa Nelson Mandela ili kujionea maandalizi ya uwanja huo kabla ya mechi ya ligi kuu baina ya Young Africans Sports Club na Tanzania Prisons itakayochezwa katika uwanja huo kabla ya mkesha wa mwaka mpya wa 2021.
Aidha aliongeza kuwa mpira ni furaha na pia ni urafiki ingawa kuna ushindani na kushinda na kushindwa ni matokeo ya mchezo na hivyo kuwakaribisha wapenzi wa mpira kutoka meneo tofauti ya ndani ya mkoa Pamoja na mikoa ya jirani ili kushuhudia historia ikitengenezwa katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga kabla yam waka 2020 kuisha.
No comments