Tetemeko la ardhi limeikumba Croatia na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Tetemeko kubwa la ardhi limelipiga eneo la katikati la Croatia leo na kusababisha athari kubwa kwa makazi na majengo katika eneo la kusini/mashariki mwa mji mkuu Zagreb.
Tetemeko hilo limemuuwa msichana wakati mwanaume mmoja na mvulana wameokolewa wakiwa katika gari iliyofukiwa na kifusi na kupelekwa hosipitali.
Kituo chenye kuhusika na masuala ya jiolojia cha Ulaya kimesema tetemeko hilo lililokumbuka eneo la kusini/mashariki mwa Zagreb lilikuwa la ukubwa wa kipimo 6.3 katika kipimo cha Richter na lilienea katika umbali wa kilometa 46.
No comments